• Call us: +255 222 666 725
  • Email: redeso-hq@redeso.or.tz
Relief to Development Society (REDESO)
SUPPORT US
  • Home
  • About Us
    • Overview
    • Vision and Mission
    • Policies and Procedures
    • Organization Structure
    • Our Partners
    • Our Team
  • Programmes
    • Child Protection
    • Education Equity and Quality
    • Health and Social Protection
    • Livelihood And Community Development
    • Natural Resources, Environment Management And Energy Solutions
  • Branches
  • News & Resources
    • News and Events
    • Reports and Publications
    • Newsletters
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
  • Contact Us

Zaidi ya Vijana na Wanawake 3,000 Kunufaika na Mafunzo ya Nishati Safi

  /   News and Resources   /   Zaidi ya Vijana na Wanawake 3,000 Kunufaika na Mafunzo ya Nishati Safi
Mar 27, 2025
Zaidi ya Vijana na Wanawake 3,000 Kunufaika na Mafunzo ya Nishati Safi
27Mar

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeingia makubaliano ya kushirikiana na Shirika la REDESO kuwapatia elimu na stadi za matumizi ya nishati safi, vijana na wanawake zaidi ya 3,000.

Hati ya makubaliano ya ushirikiano huo imesainiwa jana, tarehe 26 Machi , 2025, katika ofisi za VETA Makao Makuu jijini Dodoma ambapo mafunzo hayo yatatolewa katika vyuo vya VETA nchini.

Akizungumza baada ya zoezi la utiaji saini, Mtendaji Mkuu wa Redeso, Abeid Kasaizi, amesema pamoja na mradi huo kuwapatia ujuzi vijana na wanawake katika maeneo mbalimbali nchini kupitia mafunzo rasmi ya VETA na pia makubaliano hayo yanajumuisha mafunzo kwa walimu wa VETA kuhusu nishati safi, utayarishaji wa mitaala maalum, pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kufundishia.

"Mafunzo haya yatawasaidia kupunguza matumizi ya nishati chafu, hivyo kusaidia uhifadhi wa mazingira na kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa," amesema Kasaizi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo na kipaumbele katika matumizi ya nishati safi na kwamba VETA inaendelea kuweka na kutekeleza mipango ya matumizi ya nishati safi. 

"Sisi VETA tumeona umuhimu wa kuendeleza elimu ya matumizi ya nishati safi ili kuhakikisha wananchi wanapata ujuzi wa kuzalisha na kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira, tunatarajia kupitia mafunzo haya, wananchi wataweza kutengeneza na kutumia nishati safi na hivyo kujipatia fursa za ajira na kuchangia maendeleo endelevu ya taifa,"amesema.

Categories

  • News and Events11
  • Conferences0
  • Reports and Publications5
  • Success Stories0
  • Vacancies and Tenders0
  • Newsletters2

Other Posts

  • Apr 24, 25 Financial Statements for the Year Ending 31st December 2023
  • Nov 06, 24 REDESO na Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi na Salama Tanzania
  • May 22, 23 Turkish Embassy providing a basket charity for solidarity to Urban Refugees in Dar es salaam.
  • Dec 11, 20 Financial Regulations and Manual
  • Nov 13, 20 PSEA POLICY for REDESO

Facebook

Relief to Development Society (REDESO)

Our Address

  • 14110 Kinondoni Mjini, Mtaa wa Urambo, Dar es Salaam, Tanzania
  • redeso-hq@redeso.or.tz
  • +255 222 666 725
  • +255 717 037 311

Quick Links

  • About Us
  • Programmes
  • Our Team
  • Our Members
  • Our Partners
  • News & Events
  • Publications
  • Photo Gallery
  • Video Gallery
  • Contact Us
  • Our Locations
  • Privacy Policy

Follow Us

+255 717 037 311

By subscribing to our mailing list you will get the latest news from us.

SUPPORT US NOW

Whats New

  • Financial Statements for the Year Ending 31st December 2023
  • Zaidi ya Vijana na Wanawake 3,000 Kunufaika na Mafunzo ya Nishati Safi
  • REDESO na Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi na Salama Tanzania
  • Turkish Embassy providing a basket charity for solidarity to Urban Refugees in Dar es salaam.
  • Financial Regulations and Manual
Copyright © 2025 - Relief to Development Society (REDESO)